Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:19

Mamlaka ya Marekani ya kukagua ubora wa chakula na dawa yaidhinisha chanjo ya Covid ya Novavax


Nembo ya Chanjo ya Covid 19 ya Novavax, picha ya Reuters
Nembo ya Chanjo ya Covid 19 ya Novavax, picha ya Reuters

Mamlaka ya Marekani ya kukagua ubora wa chakula na dawa (FDA) imeidhinisha matumizi ya chanjo ya Covid 19 ya Novavax Jumatano, na hivo kuruhusu chanjo hiyo ambayo inatengenezwa kwa teknolojia ya asili ambayo ilileta matumaini kuwa itakubaliwa na watu wanaosita kupata chanjo ya Covid 19.

Baada ya taarifa hiyo, hisa za kampuni ya Novavax zimeongezeka kwa asilimia 1.3 hadi dola 70.89 baada ya dozi zake mbili kuwa chanjo ya nne ya Covid kuidhinishwa kutumiwa na watu wazima hapa Marekani.

Kituo cha Marekani cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) kinatakiwa kupitisha matumzi ya chanjo hiyo kabla ya kuigawa kwa wanainchi.

Jopo la washauri wa CDC kuhusu chanjo linatarajiwa kukutana Jumanne ijayo, lakini ratiba ya mkutano huo bado haijatolewa.

Mapema wiki hii, serikali ya Marekani ilisema ilipata dozi milioni 3.2 za chanjo ya Novavax, ambazo inapanga kuzigawa mara tu kiwanda hicho kitakuwa kimekamilisha zoezi la kupima ubora wa chanjo hiyo katika wiki chache zijazo.

Zaidi ya theluthi mbili za Wamarekani wamekwisha pata chanjo kamili ya Moderna, Pfizer au Johnson& Johnson.

Maafisa wa afya wa Marekani wanatumai kwamba watu waliopinga kudungwa chanjo ya Pfizer na Moderna ambayo inatengenezwa kwa teknolojia ya kisasa iitwayo mRNA, badala yake watakubali kudungwa chanjo ya Novavax inayotengenezwa kwa protini.

Chanjo hiyo ambayo tayari iliidhinishwa barani Ulaya, inatengenezwa kwa teknolojia ambayo ilitumiwa kwa miongo kadhaa kupambana na magonjwa kama homa ya ini na mafua.

XS
SM
MD
LG