Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:25

Mamilioni ya watu watahitaji msaada mkubwa wa chakula mwaka 2023


Mwanamme aliyebeba chakula cha msaada kilichotolewa na shirika la msalaba mwekundu, Sanaa, Yemen July 2, 2012.
Mwanamme aliyebeba chakula cha msaada kilichotolewa na shirika la msalaba mwekundu, Sanaa, Yemen July 2, 2012.

Umoja wa mataifa na washirika wake wameomba msaada wa dola bilioni 51.5 kwa ajili ya kusaidia watu kwa mahitaji muhimu mwaka ujao 2023.

Kiwango hicho cha msaada ndicho cha juu zaidi kuwahi kuombwa na umoja wa mataifa, huku idadi ya watu wanaohitaji msaada kote duniani ikiwa inaendelea kuongezeka.

Dola bilioni 51.5 ni ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na kiasi cha msaada uliotolewa mwaka 2022 na ni mara 5 ya ombi la umoja wa mataifa mwongo mmoja uliopita.

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba watu milioni 65 zaidi ya idadi ya sasa watahitaji msaada mwaka ujao.

Vita vinavyoendelea Ukraine na hali mbaya ya ukame ni miongoni mwa sababu zinazopelekea idadi kubwa ya watu kuhitaji msaada hasa wa mahitaji muhimu kama chakula.

Vita vya Ukraine vimeatatiza usafirishaji wa chakula na karibu waty milioni 45 katika nchi 37 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

XS
SM
MD
LG