Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:22

Mamia ya wanaharakati wa mazingira waandamana mjini Busan, Korea Kusini


Wanaharakati wa mazingira nchini Korea Kusini wanadai hatua kali zaidi dhidi ya taka za plastiki kwenye mazungumzo ya Umoja wa Mataifa
Wanaharakati wa mazingira nchini Korea Kusini wanadai hatua kali zaidi dhidi ya taka za plastiki kwenye mazungumzo ya Umoja wa Mataifa

Mamia ya wanaharakati wa mazingira waliandamana siku ya Jumamosi katika mji wa Busan Korea Kusini kudai kuwa na ahadi kubwa zaidi za kimataifa za kupambana na taka za plastiki.

Mamia ya wanaharakati wa mazingira waliandamana siku ya Jumamosi katika mji wa Busan Korea Kusini kudai kuwa na ahadi kubwa zaidi za kimataifa za kupambana na taka za plastiki katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa mjini humo wiki ijayo.

Takriban watu elfu moja wakiwemo wa vikundi vya asili, vijana na wakusanya taka wasio rasmi walishiriki katika mkutano huo, mratibu huyo alisema, huku baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yanayosema ondoa uzalishaji wa plastiki na punguza uzalishaji wa plastiki kwa haraka sasa.

Wanaharakati hao waliandamana kuzunguka Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Busan, ambapo kikao cha tano cha Kamati ya Majadiliano ya Kiserikali (INC-5) kitafanyika kuanzia Jumatatu kujadili makubaliano ya kisheria ya kimataifa kuhusu uchafuzi wa plastiki.

Forum

XS
SM
MD
LG