Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:31

Mameya wa zamani wa Rwanda washtakiwa nchini Ufaransa


Wakili wa Ufaransa, Richard Gisagara, ambaye anamtetea Constance Mukabazayire wa Rwanda akiwasili kwenye mahakama moja mjini Paris, Mei 10, 2016.
Wakili wa Ufaransa, Richard Gisagara, ambaye anamtetea Constance Mukabazayire wa Rwanda akiwasili kwenye mahakama moja mjini Paris, Mei 10, 2016.

Mameya wawili wa zamani wa Rwanda wamefikishwa mahakamani leo nchini Ufaransa wakikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za 1994 kwenye taifa hilo la Afrika ya kati.

Tite Barahirwa, mwenye umri wa miaka 64, pamoja na Octavien Ngenzi, mwenye umri wa miaka 58, wanatuhumiwa kuhusika moja kwa moja na mauaji wa watu 2,000 wa kabila la Tutsi waliokuwa wamechukua hifadhi kwenye kanisa moja lililoko mji wa mashariki wa Kabarondo, Aprili 13, 1994.

Walioshuhudia wanasema Barahiwa alitoa agizo akiwa ameshikilia mkuki wakati wa mkutano kwenye uwanja wa mpira la kuanza kazi ya kuuwa watutsi asubuhi ya tarehe 13 Aprili 1994.

Hata hivyo wote wawili wamekanusha mashitaka hayo, na iwapo watapatikana na hatia, basi huenda wakapewa kufungo cha maisha gerezani. Ufaransa ilipata ruhusa maalum kutoka kwa Umoja wa Mataifa ya kuongoza mashitaka dhidi ya wanaoshukiwa kutekeleza uhalifu wa kibinadamu nchini Rwanda.

XS
SM
MD
LG