Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:50

Mali yazuia uchunguzi huru wa mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na mamluki wa Russia


Wanajeshi wa Mali wakipiga doria PICHA: AFP
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria PICHA: AFP

Umoja wa mataifa umesema kwamba unasikitika sana kwamba serikali ya Mali imezuia wachunguzi wake kuingia katika mji ambapo wanajeshi na watu wanaodhaniwa kuwa mamluki wa Russia waliua mamia ya raia.

Kulingana na ripoti ya shirika linalofuatilia haki za kibinadamu la human rights watch, karibu wanaume 300 wanaaminika kuuawa kwa kupigwa risasi kati ya tarehe 27 na 31 mwezi Machi, katika mji wa Moura, wenye wakaazi karibu 10,000.

Mji huo umeingiliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Walionusurika kuuawa walisema kwamba mamluki wanaoaminika kutoka Russia walishiriki katika mauaji hayo yaliyosababisha shutuma kali kutoka kote duniani na kupelekea Umaoja wa mataifa kuanzisha uchunguzi.

Mali imekanusha madai ya kusimamisha oparesheni hiyo katika mji wa Moura na imesema kwamba itafanya uchunguzi wake.

Msemaji wa umoja wa mataida Seif Magango amesema kwamba huenda zaidi ya watu 500 waliuawa.

Kuna ripoti kwamba wanajeshi walinajisi wanawake na kuiba mali.

XS
SM
MD
LG