Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:59

Mali yapokea silaha kutoka Russia


Wanajeshi wakilipua mabomu ya kutegwa ardhini yaliyowachwa na wapiganaji
Wanajeshi wakilipua mabomu ya kutegwa ardhini yaliyowachwa na wapiganaji

Mali imepokea shehena nyingine ya silaha kutoka Russia, baada ya umoja wa ulaya kusitisha mpango wake wa mafunzo ya kijeshi katika eneo la Sahel.

Ofisi ya rais wa Mali imesema kwamba mkuu wa jeshi la Mali Maj, Gen Pumar Diarra, amepokea helikopta mbili za kivita na mitambo ya kijasusi.

Ofisi ya rais imetoa video inayoonyesha vifaa hivyo wakati vilipokuwa vinapokelewa katika uwanja wa ndege, katika mji mkuu wa Bamako. Vifaa vimesafirishwa kwa ndege ya mizigo ya Russia.

Diarra ametaja msaada huo wa Russia kwa Mali ni udhihirisho wa ushirikiano mwema sana.

Mwezi uliopita, Mali ilipokea helikopta mbili zilizotengenezwa nchini Russia, muda mfupi baada ya ripoti kwamba Waziri wa ulinzi na mkuu wa jeshi la anga kutembelea Moscow.

XS
SM
MD
LG