Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:55

Mali yaomba usaidizi wa Interpol kusaka mtoto wa Rais


Rais wa zamani wa Mali Boubacar Keita ambaye mtoto wake anasakwa.
Rais wa zamani wa Mali Boubacar Keita ambaye mtoto wake anasakwa.

Vyanzo viwili vya kisheria vya Mali vimesema Jumanne kwamba serikali imeomba kutolewa kwa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mtoto wa rais wa zamani aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacar Keita .

Keita anasakwa kutokana na kesi ya 2016 inayohusisha mwandishi wa habari aliye toweka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, idara ya polisi wa kimataifa maarufu kama interpol, ingawa haijasema lolote ina uwezo wa kutoa hati hiyo, inayoruhusu mshukiwa kukamatwa popote alipo na kurejeshwa ili kufunguliwa mashitaka.

Vyanzo kutoka mahakama moja mjini Bamako pamoja na mahakama ya rufaa vimesema kuwa mamlaka imeomba kutolewa kwa hati ya kimataifa itakayo wezesha kukamatwa kwa Karim Keita bila kutoa taarifa zaidi.

Baraza la waandishi wa habari kutoka mataifa ya Afrika magharibi limesifu hatua ya kumsaka Keita ambaye anasemekana kutorokea Ivory Coast tangu mapinduzi ya Agosti yaliomuondoa baba yake madarakani.

Mkuu wa baraza hilo Bandiougou Dante amesema hatua hiyo huenda ikafichua kulichomfanyikia mwandishi wa kijasusi Birama Toure aliyetoweka Januari mwaka wa 2016.

XS
SM
MD
LG