Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:47

Mali yaomba msaada wa jeshi kutoka ECOWAS


Wapiganaji wa makundi ya ki-Islam wakiwa kwenye kifaru karibu na uwanja wa ndege wa Gao, Mali, August 7,2012
Wapiganaji wa makundi ya ki-Islam wakiwa kwenye kifaru karibu na uwanja wa ndege wa Gao, Mali, August 7,2012

Makundi ya wanamgambo yalichukua udhibiti upande wa kaskazini mwezi April baada ya wanajeshi waasi walipoipindua serikali katika mji mkuu Bamako

Afisa mmoja wa Ufaransa anasema Mali imewaomba rasmi majirani zake wa Afrika magharibi kusaidia kuwaondoa wanamgambo wa ki-Islam kutoka upande wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwakilishi maalumu wa Ufaransa kwa eneo la Sahel, Jean Felix-Paganon anasema Mali imeiomba jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi-ECOWAS kupeleka msaada wa kijeshi ili kuleta uthabiti katika nchi na hasa kulikamata tena eneo la kaskazini.

Afisa huyo aliwaambia waandishi wa habari jumanne jioni kwamba alifahamu kuhusu ombi hilo wakati wa mkutano katika mji mkuu wa Burkina Faso na Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore.

ECOWAS inasema iko tayari kupeleka jeshi nchini Mali lenye wanajeshi wapatao 3,000 ambako makundi ya wanamgambo wa ki-Islam yanajaribu kulazimisha sheria kali za ki-islam.

Moja ya makundi hayo ni Movement for Oneness na Jihad in West Africa, waliteka mji mwingine wiki hii na kukaribia eneo linalodhibitiwa na serikali ya muda ya Mali.

Makundi hayo yalichukua udhibiti wa upande wa kaskazini mwezi April baada ya wanajeshi waasi walipoipindua serikali iliyochaguliwa katika mji mkuu, Bamako.

Marekani na Umoja wa Mataifa wanalaani hatua za wanamgambo na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanasema hatua za wanamgambo zimezidisha matatizo ya kibinadamu katika eneo lililosababishwa na hali ya ukame na kupanda kwa bei za chakula.

Serikali ya muda nchini Mali inaapa kulikamata tena eneo la kaskazini.
XS
SM
MD
LG