Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 08:20

Uchaguzi Mali waingia duru ya pili


Wagombea wa urais kutoka vyama vya upinzani nchini Mali

Kiongozi mkuu wa upinzani mali , Soumaila Cisse amesma hatambui matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa jana ambapo rais Ibrahim Boubacar Keita alitangazwa mshindi.

lakini kiongozi huyo hakuweza kupata zaidi ya asilimia 50 za kura kuweza kushinda uchaguzi huo moja kwa moja.

Kutokana na matokeo hayo ambapo Keita alipata asilimia 41.42 , atashindana katika duru ya pili Agosti 12 dhidi ya Cisse aliyepata asili mia 11.8.

Kiongozi huyo wa upinzani anasema matokeo hayo hayakubaliki kwa sababu yalikuwa na wizi wa kura na katika vituo kadhaa masanduku ya kura yalikuwa na kura tayari kabla ya kuanza kwa upigaji kura.

Kulikuwepo na wagombea 24 katika uchaguzi wa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi linalo kabiliwa na misukosuko kutokana na mashambulizi ya kigaidi.

Hii itakua mara ya pili kwa Rais Keita kupambana na Cisse katika duru ya pili kama ilivyo tokea katika uchaguzi wa 2013.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG