Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 08:06

Waasi wa Mali watakiwa kukata uhusiano na magaidi


Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Fasso, Djibril Bassole.
Mpatanishi wa Afrika Magharibi amewaambia waasi kaskazini mwa Mali lazima wajitenge na magaidi kabla ya mazungumzo ya amani kuanza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Djibril Bassole, ambaye anaiwakilisha Jumuiya ya uchumi ya mataifa ya Afrika Maghairbi - Ecowas, alitembelea eneo la kaskazini mwa Mali na kukutana na viongozi wa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Ansar Dine katika mji wa Kidal.

Akiongea na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Burkina Faso baada ya safari yake, Bassole amesema amewaeleza waasi juu ya matakwa ya Ecowas.

Amesema pia aliutembelea mji wa Gao, ambao unadhibitiwa na kundi jingine la wanamgambo la MUJAO. Alizungumza na viongozi wa eneo hilo lakini si wa kundi la MUJAO.

Ecowas inaongoza juhudi za kieneo kusuluhisha mzozo wa kisiasa wa Mali, ambao ulianza pale wanajeshi walipoiangusha serikali mwezi Machi, na kuwaruhusu waasi kulikamata eneo la kaskazini mwa nchi.
XS
SM
MD
LG