Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:10

Magaidi washambulia hoteli ya kifahari Mali


Vikosi vya usalama karibu na hoteli iliyoshambuliwa mjini Bamako Mali, Nov. 20, 2015.
Vikosi vya usalama karibu na hoteli iliyoshambuliwa mjini Bamako Mali, Nov. 20, 2015.

Maafisa wa Mali wanasema watu wanne waliokuwa na bunduki na kushambulia hoteli ya kifahari katika mji mkuu wa nchi hiyo mapema leo wameua watu 3 kati ya mateka wao 170 waliowashikilia.

Mamlaka zinasema karibu mateka 20 wameachiliwa huku baadhi yao wakichukuliwa na magari ya wagonjwa.

Mapema leo ripoti zinasema watu hao wenye silaha wamewachia watu walioweza kusoma Quran. Maafisa wanasema vikosi vya Umoja wa Mataifa na Mali walikuwa wameizunguka hoteli iliyovamiwa, na barabara kuelekea huko zimefungwa.

Mali imewaambia wananchi kuwa watulivu na kubaki katika sehemu walipo

XS
SM
MD
LG