Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:27

Malaysia huenda ikafunga ofisi za UNHCR nchini


Wakimbizi wa Rohingya wakiondoka Myanmar kwenye picha ya awali.
Wakimbizi wa Rohingya wakiondoka Myanmar kwenye picha ya awali.

Malaysia imesema kwamba inatadhimini kufunga ofisi ya Umoja wa mataifa ya kushughulikia wakimbizi nchini humo wakati kukiwa na tetesi kwamba serikali inalazimisha waomba hifadhi wa Myanmar waliyokimbilia usalama  kurejea makwao.

Utawala wa kijeshi uliyochukua madaraka nchini Myanmar mapema mwaka jana umesema kwamba Malaysia imerejesha mamia ya raia wake kwa ndege za kukodisha katika miezi ya karibuni , ukiongeza kuwa wengi wao wanarejea bila hiari .

Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yanadai kwamba Malaysia inawalazimisha kurejea baada ya kukamatwa kwa kigezo cha kuwa nchini humo kinyume cha sheria.

Kuna hofu kwamba baadhi ya waomba hifadhi watakamatwa, kuteswa au hata kuuwawa baada ya kurejea Myanmar. Jeshi la taifa hilo linalaumiwa kwa kukamata na kuuwa maelfu ya raia wake, kama juhudi ya kunyamazisha wanaopinga utawala wake.

XS
SM
MD
LG