Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:04

Malawi tayari kwa uchaguzi mkuu: SADC


Wafuasi wa Rais Joyce banda anaepigania kiti chake wamshangiria katika kampeni yake ya mwisho katika kijiji cha Songani nje ya nmji wa Zomba, mji mkuu wa zamani wa Malawi, May 17, 2014.
Wafuasi wa Rais Joyce banda anaepigania kiti chake wamshangiria katika kampeni yake ya mwisho katika kijiji cha Songani nje ya nmji wa Zomba, mji mkuu wa zamani wa Malawi, May 17, 2014.
Kampeni za uchaguzi wa rais wa nchini Malawi zimemalizika rasmi Jumapili kabla ya uchaguzi mkuu tarehe 20 May. Vyama vya kisiasa vilikamilisha kapmeni zao kwa kuanda mikutano mikubwa ya hadhara katika miji mbali mbali ya nchi hiyo.

Kuna wagombea 12 wa kiti cha rais, katika uchaguzi unaoaminika utakuwa ushindani kabisa kuwahi kutokea tangu kunaza kwa mfumo wa vyama vingi mwanzoni wa miaka ya 90.

Rais Joyce Banda aliyechukua madaraka baada ya kufariki kwa Rais Bingu wa Muitharika mwaka 2012, alimaliza kampeni yake katika wilaya alikozaliwa ya Zomba akitoa wito kwa Wamalawi kumchagua kwa mhula kamili kuweza kukamilisha miradi aliyoanzisha ya kuimarisha uchumi wa nchi yake.

Hata hivyo Bi Banda aliyeingia madarakani akiwa mashuhuri kwa kuanza kukabiliana na rushwa anakabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani ambapo kufuatana na uchunguzi wa maoni wa wiki hii alikua anashikilia nafasi ya tatu.

Ujumbe wa wafuatiliaji kutoka Jumuia ya Maendeleo ya Kusni mwa Afrika SADC, unaeleza kwamba unaridhika na matayarisho kutokana na maelezo kutoka tume ya uchaguzi ambayo imewahakikishia ucahguzi utafanyika kwa njia ya Amani, uwazi na haki.
XS
SM
MD
LG