Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:55

Maandamano nchini Malawi yavurugwa na polisi


Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika
Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika

Polisi nchini Malawi wamepambana na waandamanaji katika miji mikubwa Jumatano wakati wa maandamano dhidi ya utawala mbaya na kudidimia kwa uchumi.

Viongozi wa kiraia na mashahidi wanasema polisi waliingia kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Lilongwe, mji wa kibiashara wa Blantyre na mji wa Mzuzu.

Waandamanaji ambao wengi walivalia nguo nyekundu walijitokeza mitaani licha ya amri ya mahakama Jumanne jioni kupiga marufuku maandamano yanayoipinga serikali. Mashahidi wanasema waandamanaji wenye hasira wamechoma moto katika miji ya Lilongwe na Mzuzu wakati polisi huko Blantyre wakifyatua mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya waandamanaji.

Hali inasemekana kuwa tete nchini humo ambapo waandamanaji wanaelezea hasira juu ya sera za Rais Bingu wa Mutharika. Wakosoaji wa masuala ya kisiasa wanamlaumu kiongozi huyo kwa kuongeza bei, kudharau umoja na sera mbovu za serikali.

Bwana Mutharika anakosolewa namna anavyokabiliana na mzozo wa kidiplomasia ambao ulichochea Uingereza kukata msaada wa kiuchumi kwa taifa hilo ambalo ni koloni lake la zamani.

Mzozo ulianza baada ya Rais Mutharika kumfukuza nchini humo mwakilishi wa Uingereza akimuelezea kuwa mtu aliyetoa taarifa nyeti kama hatari na hawezi kuvumiliwa.

Maandamano ya nchi nzima yalipangwa na makundi ya ushirika ya kiraia na haki za binadamu pamoja na vyama vya upinzani.


XS
SM
MD
LG