Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:46

Malawi inaomboleza kifo cha Rais Mutharika


Makamu wa rais wa Malawi Joyce Banda akiongea na vyombo vya habari katika mji mkuu Lilongwe.
Makamu wa rais wa Malawi Joyce Banda akiongea na vyombo vya habari katika mji mkuu Lilongwe.

Wananchi wa Malawi watakiwa wawe na utulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.

Makamu wa rais wa Malawi, Joyce Banda ameomba kuwepo kwa utulivu wakati taifa linaomboleza kifo cha marehemu rais Bingu wa Mutharika, ambaye alifariki kwa mshtuko wa moyo.

Bi Banda aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi kwamba benderea zitapepea nusu mlingoti na kwamba vyombo vya habari televisheni na radio vipige nyimbo za majonzi katika muda wa siku 10 zijazo.

Radio ya taifa ya Malawi imethibitisha mapema Jumamosi kwamba rais Mutharika amefariki, baada ya siku mbili ya kuwepo na habari ambazo hazijathibitishwa.

Katiba ya Malawi inaelezea kwamba makamu wa rais atachukua mamlaka ya urais kama rais atafariki, lakini Bi Banda bado hajaapishwa kushika wadhifa huo.

XS
SM
MD
LG