Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:33

Malaria yapungua Tanzania


Aina ya mbu waenezao ugonjwa wa Malaria
Aina ya mbu waenezao ugonjwa wa Malaria

Hayo yameelezwa Jumatano jijini Dare s salaam na wataalamu wa masuala ya afya, wakati wa uzinduzi wa ripoti maalumu juu ya hali ya ugonjwa wa malaria

Tanzania imeanza kupata mafanikio kwenye juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa malaria, ugonjwa ambao unatajwa kusababisha vifo vingi.

Hayo yameelezwa Jumatano jijini Dare s salaam na wataalamu wa masuala ya afya, wakati wa uzinduzi wa ripoti maalumu juu ya hali ya ugonjwa wa malaria, tangu kuasisiwa kwa azimio la Abuja la mwaka 2000 lililopitishwa na viongozi wa umoja wa Africa.

Wataalamu wa afya wanasema kwamba, mafanikio zaidi yameanza kujitokeza kwa makundi ya kina mama wajawazito na watoto waliochini ya umri wa miaka 5, ambao ndiyo wanachukua asilimia kubwa ya kuugua ugonjwa huo na hatimaye kupoteza maisha.

Takwimu za hivi sasa zinaonyesha kuwa, karibu watanzania milioni 11 wameugua ugonjwa huo, na jambo la kusikitisha ni kwamba kila mwaka watu 38,000 hupoteza maisha kutokana na malaria.

Katika nasaha zake wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Makamu wa Rais Dr Ghalib Bilal alitaja shabaha ya serikali katika siku za usoni kujenga kituo maalumu kitakachozalisha dawa za kukabiliana na masalia ya mbu waenezao malaria.

Wakati kukitajwa kuanza kupatikana mafanikio kwenye juhudi hizo za kukabili ugonjwa wa malaria, hata hivyo nchini nyingi za kiafrika ambazo zinachukua asilimia 80 ya vifo vyote vya malaria dunia, zinakabiliwa na tatizo la uhaba wa mafungu ya fedha. Miradi mingi ya kiafya inashindwa kuendelezwa kutokana na uwekezaji mdogo unaofanywa kwenye sekta hiyo ya afya.

Kwa kulitambua tatizo hilo, mwakilishi wa shirika la afya ulimwenguni WHO, Dr Robert Chatola, ametoa mwito akitaka kuwepo mafungamano ya pamoja na kuongeza uwekezaji kwenye sekta hiyo ya afya.

Kwa kiwango kikubwa Zanzibar inasalia eneo pekee katika ukanda wa afrika mashiriki kupata mafanikio makubwa ya upunguzaji wa vifo vitokanavyo na malaria.

XS
SM
MD
LG