Taarifa imesema hatua hiyo inafuatia mkutano kati ya viongozi wa makundi yenye silaha na kiongozi wa mpito Ahmad al-Sharaa, aliyewaongoza waasi waliomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Assad.
Waasi waliudhibiti mji mkuu wa Damascus Desemba 8, baada ya kudhibiti miji mingine ya Syria baada ya miaka 13 ya mapigano na kupelekea utawala wa Assad kuanguka.
Tangu Assad kuondoka madarakani, serikali kadhaa katika kanda hiyo ya Mashariki ya Kati zimetuma wajumbe mjini Damascus kujadili hali ya baadaye ya Syria na utulivu wa kanda hiyo.
Kati ya maswala yanayozungumziwa zaidi ni uwezekano wa kurudi tena kwa kundi la Islamic State, ambalo lilidhibiti sehemu za mashariki mwa Syria hapo mwaka 2014, na magharibi mwa Iraq kabla ya kupoteza udhibiti wake.
Forum