Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 14:25

Makundi ya waasi yamepigana mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa DRC wakishika doria katika sehemu ambayo ilishambuliwa na waasi wa M23. Picha: Austere Malivika
Wanajeshi wa DRC wakishika doria katika sehemu ambayo ilishambuliwa na waasi wa M23. Picha: Austere Malivika

Mapigano makali yametokea kati ya waasi wa kundi la M23 na makundi mengine ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kundi la M23, ambalo wapiganaji wake wanatoka kabila la Watutsi, linadhibithi sehemu kubwa ya mkoa wa Kivu kaskazini, mashariki mwa Congo, na lilitishia kudhibithi mji wa Goma.

Kulingana na vyanzo vya habari katika makundi ya waasi, mapigano kati ya M23 na makundi pinzani, yametokea katika sehemu ya Tongo, kivu kaskazini.

Dominique Ndaruhutse, kamanda wa kundi la waasi la CMC/FDP, amesema kwamba wapiganaji 13 wa kundi la M23 wameuawa katika makabiliano hayo.

Msemaji wa kundi la CMC/FDP, ambalo ni muungano wa makundi kadhaa ya waasi Jules Mulumba, amesema kwamba wapiganaji wanne wa upande wao wamejeruhiwa.

Hatujadhibitisha idadi hiyo ya vifo.

Mulumba amesema kwamba wanapigana na M23 ili kulinda nchi yao na kwamba hawataruhusu kuwa watumwa nchini mwao, akisisitiza kwamba M23 wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda, madai ambayo Rwanda imekanusha kila mara.

Mulumba amesema kwamba kundi la M23 lilitaka kudhibithi sehemu yam ji wa Kitshanga, kilomita 125 magharibi mwa Goma.

Kuna zaidi ya makundi 120 ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

XS
SM
MD
LG