Makundi ya timu zitakazo shiriki fainali za mataifa ya Afrika yamepatikana katika droo iliyofanyika Malabo, Equatorial Guinea, ambapo michuano hiyo itafanyika kuanzia January 17 mpaka Febuari 8 mwakani.
Droo hiyo iliyohudhuriwa na wawakilishi wa timu zilizofuzu michuano hiyo na viongozi wanachama wa shirikisho la soka barani Afrika CAF kutoka karibu pande zote za Afrika.
Michano kama hii haikosi kundi la “kifo,” kundi C linapewa jina hilo kwa kuwa linakutanisha timu mahiri za Ghana, Algeria, Senegal na Afrika Kusini. Ni vigumu kutabiri nani atasonga mbele ama nani atabaki.
Droo hiyo ilimalizika kwa kutoa makundi manne kama ifuatavyo.
Kundi A: Equatorial Guinea, Burkina Faso, Congo, Gabon
Kundi B: Zambia, Cape Verde Islands, Democratic Republic of Congo, Tunisia
Kundi C: Ghana, Algeria, Senegal, Afrika Kusini
Kundi D: Ivory Coast, Cameroon, Guinea, Mali