Ushirika wa kundi la haki za binadamu umetoa wito kwa viongozi wa Umoja wa Afrika siku ya Alhamis kupuuza kufikiria mipango ya kutaka kuondoa wanachama wake kutoka mahakama ya uhalifu wa kimataifa-ICC.
April mwaka jana kamati iliyokutana ndani ya Umoja wa Afrika-AU ilishauri kujitoa uanachama kutoka ICC kama isipofikia masharti matatu mojawapo ilikuwa kinga ya kutowashitaki wakuu wa nchi na maafisa waandamizi wengine.
Ushirika huo unaoongozwa na kundi la haki za binadamu la Human Rights Watch lenye makao yake nchini Marekani lilisema wito huu wa kinga unakiuka kipengele cha katiba ya Umoja wa Afrika na inakwenda kinyume na juhudi za karibuni za Umoja wa Afrika zenye lengo la kutokomeza rushwa. Makundi hayo ya haki za binadamu yanasema kinga kwa wakuu wa nchi haijawahi kuwa mwongozo kwa mahakama ya kimataifa na uamuzi wa kujitoa kutoka mahakama ya kimataifa unatakiwa kuamuliwa na nchi moja moja.