Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:13

Serikali ya Sudan Kusini na upinzani watofautiana juu ya kuapishwa makamu rais mteule


Kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini, Riek Machar akiongea na waandishi wa habari kabla ya kurejea Juba kushika wadhifa wa makamu rais.
Kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini, Riek Machar akiongea na waandishi wa habari kabla ya kurejea Juba kushika wadhifa wa makamu rais.

Huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya makamu rais mteule wa Sudan Kusini, Riek Machar, kurudi katika mji mkuu, serikali na upinzani bado wanalumbana juu ya namna kiongozi huyo wa waasi atakavyokaribishwa na lini ataapishwa.

Msemaji wa upinzani wa SPLM-IN, William Ezekiel amesema matumaini ya chama chake ni kwamba kiongozi wao bado atawasili mjini Juba siku ya Jumatatu, lakini alisema pande hizo mbili bado hazijafanya kazi ya kuandaa mapokezi ya Machar.

Alisema kwamba huu ni wasi wasi wa upande wetu, lazima aapishwe siku anayowasili, hali ya dharura lazima iondolewe na uonodoaji wa majeshi mjini juba ni vyema uthibitishwe na CTSAMM.

XS
SM
MD
LG