Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 01:09

Makombora ya Russia yaharibu mitambo muhimu ya umeme na maji Ukraine


Ndege isiyo na rubani muda mfupi kabla ya kushambulia jengo mjini Kyiv, Okt 17 2022
Ndege isiyo na rubani muda mfupi kabla ya kushambulia jengo mjini Kyiv, Okt 17 2022

Makombora ya Russia yameharibu mitambo ya umeme na maji katika sehemu kadhaa nchini Ukraine leo Jumanne, katika hatua inayoonekana kama wanajeshi wa Russia kuharibu mifumo muhimu ya Ukraine kwa makusudi wakati msimu wa baridi unapoanza.

Meya wa mji wa Zhytomyr, wenye watu 263,000 amesema kwamba mashambulizi ya makombora yameharibu mitambo ya maji na umeme.

Mashambulizi mengine mawili yamepiga mtambo wa nishati Kusini Mashariki katika mji wa Dnipro wenye wakazi karibu milioni 1, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Mtu mmoja amefariki kufuatia shambulizi la kombora lililopiga jengo linalokaliwa na watu katika mji wa bandari wa Mykolaiv, kusini mwa Ukraine, huku mengine yakipiga majengo katika mji mkuu wa Kyiv.

Kukatika kwa umeme, maji wakati kipindi cha baridi kinaanza

Kuna ripoti za makombora kulenga mitambo ya nishati katika mji wa Kharkiv ulio karibu na mpaka na Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensiky ameishutumu Russia kwa kuua raia kutokana na mashambulizi ya makombora mjini Kyiv na miji mingine.

Hakuna idadi kamili ya watu waliouawa kutokana na mashambulizi ya makombora ya Russia nchini Ukraine.

Mashambulizi ya Russia yanaongozwa na Jenerali Sergei Suvorikin aliyeongoza operesheni ya Russia nchini Syria na Chechnya.

Uteuzi wake kuongoza uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulifuatiwa na mashambulizi ya kila mara ya makombora ya ndege zisizokuwa na rubani, tangu Moscow ilipoivamia Ukraine Februari 24.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kwamba mashambulizi yake yanalenga wanajeshi wa Ukraine na mifumo muhimu ya nshati na wala siyo raia

XS
SM
MD
LG