Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 23:38

Makombora ya Russia karibu na kiwanda cha nyuklia Ukraine yapelekea hofu


Wafanyakazi wakitengeneza mfumo wa umeme katika kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia Ukraine. Agosti 22, 2022. REUTERS/Alexander Ermochenko.

Russia ilifyatua makombora  katika miji ya Ukraine iliyo  karibu na   kiwanda cha nyuklia cha Zapori-zhzhia usiku kucha, maafisa wa eneo hilo walisema siku ya Jumapili, na kuongeza wasiwasi kwa wakaazi huku ripoti za makombora kuzunguka mtambo huo zikizidisha hofu ya maafa ya kuvuja kwa  mionzi.

Wizara ya ulinzi ya Russia ilidai siku ya Jumapili kwamba kulikuwa na mashambulizi zaidi ya Ukraine kwenye mtambo huo katika muda wa saa 24 zilizopita, siku moja tu baada ya Moscow na Kyiv kushutumiana kila upande ikilenga kiwanda kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, jambo ambalo limezua wasiwasi mkubwa wa kimataifa.

Kampuni ya nyuklia ya Ukraine Energ-oatom ilisema haina taarifa mpya kuhusu mashambulizi kwenye kiwanda hicho.

Kiwanda hicho kilitekwa na wanajeshi wa Russia mwezi Machi, lakini bado kinaendeshwa na wafanyakazi wa Ukraine, eneo hilo la mstari wa mbele wa kusini wa vita limekuwa moja ya changamoto kuu za mzozo huo uliodumu kwa miezi sita.

Gavana wa mkoa Oleksandr Starukh alisema kwenye Telegram siku ya Jumapili kwamba vikosi vya Russia vilipiga majengo ya makazi katika mji mkuu wa mkoa wa Zaporizhzhia, karibu saa mbili kwa gari kutoka kwenya kiwanda hicho, na mji wa Orikhiv upande wa mashariki.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG