Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 00:56

Makamu wa rais wa Argentina apatikana na hatia ya ubadhilifu wa fedha.


Makamu rais wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner .Nov. 17, 2022.
Makamu rais wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner .Nov. 17, 2022.

Makamu wa rais wa Argentina Christina Fernandez de Kirchner, Jumanne amepatikana na hatia ya ubadhirifu wa dola bilioni moja za kimarekani, alizopokea wakati wa kutoa kandarasi za umma akiwa mamlakani.

Jopo la majaji watatu limemkuta na hatia na kumpa kifungo cha miaka 6 jela, huku akizuiliwa kushika nafasi za kuongoza umma katika maisha yake. Hii ni mara ya kwanza kwa makamu wa rais wa Argenitina kuhukumiwa wakati akiwa ofisini.

Akizungumza muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa, de Kirchner amelitaja jopo hilo kuwa ni "mafia ya mahakama," wakati akitarajiwa kukata rufaa. Hukumu yake haiwezi kutekelezwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa, na huenda ikachukua miaka kadhaa.

Kulingana na sheria za Argentina, kiongozi huyo pia hawezi kukamatwa, mradi ataendelea kuchaguliwa na wananchi. Wafuasi wake wameapa kusimamisha shughuli za kawaida kote nchini kupitia maandamano.

XS
SM
MD
LG