Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:15

Majimbo matano yanafanya uchaguzi wa awali Marekani


Wagombea urais wanaoongoza Marekani, Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat. March 1, 2016.
Wagombea urais wanaoongoza Marekani, Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat. March 1, 2016.

Wapigaji kura katika majimbo matano ya Marekanio wanashiriki katika uchaguzi muhimu wa awali siku ya Jumanne ambao utaweza kutoa ishara kamili za nani huwenda akawa mgombea wa kiti cha rais wa vyama vya Republican na Democratic.

Uchaguzi huo unaofanyika katika majimbo ya Florida, Illinois, Missouri, North Carolina na Ohio umekua wa kipekee kwani kwa kawaida kufikia wakati huu miaka ya nyuma ishara ya mshindi hujitokeza wakati wa uchaguzi wa awali unaofanyika Jumanne ya kwanza ya mwezi wa Machi, lakini katika mwaka huu hadi hivi sasa haijulikani nani ataongoza na ndio maana ya kupatiwa jina la “SUPER TUESDAY 3”.

Kwa upande wa wagombea wa Republican uchaguzi huu huwenda ikawa fursa ya mwisho kwa wagombea watatu waliyo nyuma ya mgombea anaeongoza tajiri Donald Trump kubadili hali ya mambo na kumzuia asiweze kua na idadi ya wajumbe wanaohitajika kuweza kuteuliwa na mkutano mkuu wa chama mwezi Julai.

Halikadhalika kwa upande wa Democrat hali bado ni ya kitendawili kati ya wagombea Hillary Clinton anaeongoza idadi ya wajumbe mbele ya mpinzani wake Bernie Sanders ambae anaweza pia kubadili hali ya mambo akipata ushindi katika majimbo kadhaa.

Akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA mkuu wa idara ya fasihi za dunia na lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha Georgia hapa Marekani, Dr. Lioba Moshi alisema, “Ni jimbo ambalo lina mchanganyiko wa wahamiaji, kuna wahamiaji wanaotoka Amerika ya kusini walio wengi hasa waliotoka Cuba na Mexico, umuhimu mwingine ni kwamba jimbo hili lilikuwa na utata katika uchaguzi wa siku za nyuma wa Gore na Bush hivyo bado kuna mawazo ya kwamba kwa sababu ya kikundi kikubwa cha watu weusi na wako sehemu moja itaonekana kazi kubwa kuchanganua wapigaji kura”

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:11 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Florida ndilo jimbo muhimu kwa uchaguzi wa Jumanne kwa upande wa Republican kwani mshindi anapata wajumbe wote 99. Na Seneta wa jimbo hilo Marco Rubio analazimika kushinda ikiwa anataka kubaki katika mashindano, lakini uchunguzi wa maoni wa mwisho unaonesha Trump akiwa anaongoza kwa angalau asilimia 17.

Jimbo jingine muhimu la kufuatilia ni Ohio ambako Gavana wake John Kasich anaongoza katika uchunguzi wa maoni na amepata uungaji mkono wa spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Bunge, John Boehner.

Kwa upande wa Wa-democrat, Bi. Clinton aliyekua waziri wa mambo ya nchi za nje anaongoza katika majimbo ya Florida na North Carolina huku akikabiliwa na ushindani mkali huko Illinois, Ohio na Missouri.

XS
SM
MD
LG