Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 19:45

Maji yagunduliwa Turkana, Kenya


Eneo kavu la Turkana kaskazini mwa Kenya
Eneo kavu la Turkana kaskazini mwa Kenya
Wanasayansi wametangaza kupata chanzo kikubwa cha raslimali ya maji katika eneo kavu na masikini sana la Turkana kaskazini mwa Kenya.

Ugunduzi huo ulitangazwa Jumatano kufuatia utafiti wa teknolojia ya satellite uliofanywa na shirika la kimataifa la elimu na sayansi UNESCO kwa ushirikiano na serikali ya Kenya.

Utafiti huo uligundua mabwawa mawili makubwa na yenye maji mengi chini ya ardhi huko Turkana yakiwa na ukubwa cubic mita bilioni 250 za maji yanayokisiwa kuwa maradufu kiasi cha maji Wakenya wanayotumia.

Wanasayansi hao wanasema uchunguzi zaidi utafanywa kubaini usalama wa maji hayo. Umoja wa Mataifa unasema Wakenya milioni 17 au asili mia 40 hawana maji safi ya kunywa.

Nao maafisa wa Kenya wamesema ugunduzi huo utasaidia serikali kuhudumia raia wa eneo la Turkana ambalo ni kavu pamoja na maeneo mengine ya nchi yenye utashi mkubwa wa maji.

Eneo la Turkana limo kaskazini mwa Kenya na linapakana na Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia.
XS
SM
MD
LG