Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:12

Majeshi ya usalama ya Syria yaua waandamanaji


Waandamanaji wamekusanyika katika mji wa kusini wa Daraa, baada ya sala ya Ijumaa.
Waandamanaji wamekusanyika katika mji wa kusini wa Daraa, baada ya sala ya Ijumaa.

Watu 38 wauawa na majeshi ya usalama wakati wa maandamano ya Ijumaa kote nchini humo.

Wanaharakati wa haki na baadhi ya mashahidi wanasema majeshi ya usalama ya Syria yamewafyatulia risasi waandamanaji wanaoipinga serikali ya nchi hiyo na kuua watu 38.

vifo, ambavyo vimeripotiwa kutokea kote nchini humo, huenda vikaifanya Ijumaa ya leo ni siku ya kutisha zaidi tangu maandamano yaanze nchini Syria mwezi Machi mwaka huu.

Matukio yameripotiwa baada ya maelfu ya waandamanaji kote nchini Syria kuingia mitaani kumtaka rais Bashar al-Assad aondoke haraka madarakani. Majeshi ya usalam yalijibu kwa kutumia risasi za moto na gesi ya machozi.

Ripoti zinasema vifo vingi vimetokea katika mkoa wa kusini wa Daraa, kiini cha maandamano ya karibuni. Mashirika ya habari yanasema mashahidi pia wameripoti vifo katika eneo moja la mji mkuu Damascus, na mji wa kati wa Homs.

Maandamano ya Ijumaa dhidi ya serikali ya rais Assad yamekuja siku moja baada ya rais kutia saini amri inayomaliza sheria ya dharura iliyodumu kwa takriban miaka 50. Amri hiyo ilikuwa sehemu ya juhudi za rais kumaliza ghasia dhidi ya serikali.

Hakuna uthibitisho uliopatikana kuhusu vifo hivyo kutoka kwa maafisa wa Syria. Shirika la habari la serikali SANA limesema polisi na majeshi ya usalama walitumia gesi ya machozi na mabomba ya maji hivi leo baada ya vurugu kuzuka kati ya waandamanaji na raia.

XS
SM
MD
LG