Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:39

Majeshi ya Sudan Kusini yawabughudhi raia-Amnesty International


Wanajeshi wa Jeshi la Sudan Kusini-SPLA
Wanajeshi wa Jeshi la Sudan Kusini-SPLA

Jeshi lilizindua kampeni ya kutokomeza silaha mwanzoni mwa mwaka huu baada ya wimbi la ghasia za kikabila katika jimbo la Jonglei.

Shirika la Amnesty International linasema majeshi ya usalama ya Sudan Kusini yametenda ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu huku wakifanya kampeni ya kuwapokonya silaha raia katika jimbo la Jonglei.

Kundi lilisema katika ripoti ya Jumatano kuwa ukiukaji unaofanywa na wafanyakazi wa polisi na jeshi unajumuisha unyanyasaji, ufyatuaji risasi na ghasia za ngono.

Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa mahojiano na watu katika wilaya ya Pibor. Mwezi Agosti, Human Rights Watch na ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini zilishutumu ukiukaji kama huo katika eneo hilo hilo.

Maafisa walikanusha ripoti za awali kuwa za kisiasa na zenye uchochezi wakisema shutuma hizo zimetiwa chumvi.

Amnesty International, Jumatano iliitaka Sudan Kusini kufanya uchunguzi huru na wa wazi kuhusiana na shutuma za unyanyasaji. Pia iliisihi ofisi ya Umoja wa Mataifa kuongeza juhudi zake za kuwalinda raia.

Jeshi lilizindua kampeni ya kutokomeza silaha mwanzoni mwa mwaka huu baada ya wimbi la ghasia za kikabila kati ya makabila ya Lou Nuer na Murle katika jimbo la Jonglei.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba zaidi ya watu 600 walikufa baada ya maelfu ya vijana wenye silaha wa kabila la Lou Nuer, pamoja na baadhi ya wakazi wa kabila la Dinka kuvamia vijiji huko Pibor County. Kiasi cha watu 300 wengine waliuwawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
XS
SM
MD
LG