Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 01:38

Majeshi ya Somalia yachukua mji mwingine


Mpiganaji wa jeshi la serikali ya Somalia.

Serikali ya Somalia imesema majeshi yake yamechukua tena udhibiti wa mji wa Bula Hawo.

Serikali ya Somalia imesema majeshi yake yamechukua tena udhibiti wa mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya kutoka kwa waasi wa Kiislam.

Wizara ya habari inasema majeshi ya serikali yaliteka mji wa Bula Hawo jumapili baada ya kushambulia wapiganaji wa kundi la al-Shabab.

Mapigano zaidi yameripotiwa Beledweyne, mji mmoja ulio mpakani mwa Somalia na Ethiopia. Serikali imesema mapigano hayo yametokana na mashambulizi yaliyolenga kuchukua upya miji inayodhibitiwa na al-Shabab katika maeneo matatu tofauti.

Maafisa wanasema wapiganaji 11 wa al-Shabab na askari mmoja wa serikali waliuwawa katika mapigano ya Bula Hawo. Majeshi hayo yakiongozwa na mbunge mmoja wa Somalia, Barre Hirale, ambaye aliwahi kuongoza kikosi cha kijeshi cha kikabila siku za nyuma.

XS
SM
MD
LG