Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:33

Majeshi ya AU yaendeleza mashambulizi Somalia


Wakimbizi wa njaa eneo la Kusini mwa Somalia kwenye wilaya ya Hodan Mogadishu.
Wakimbizi wa njaa eneo la Kusini mwa Somalia kwenye wilaya ya Hodan Mogadishu.

Majeshi ya Umoja wa Afrika yanapambana na Alshabab katika juhudi za kusaidia kusambaza chakula cha misaada.

Majeshi ya Umoja wa Afrika yanaendelea na mashambulizi huko Somalia katika juhudi za kurahisisha usafirishaji wa chakula cha misaada katika nchi hiyo iliyokumbwa na janga la njaa.

Msemaji wa jeshi la kulinda amani la AU Paddy Akunda aliiambia VOA kwamba vikosi vinajaribu kuukamata uwanja wa mpira wa Mogadishu na maeneo mengine muhimu yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Alshabab.

Alshabab wamekana kwamba kuna njaa nchini humo na kupiga marufuku mashirika mengi ya misaada kufanya kazi katika maeneo ya kusini na kati ya Somalia.

XS
SM
MD
LG