Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 06:13

Majambazi wenye silaha waua watu 135 Nigeria


Nigeria

Watu wenye silaha katika darzeni za pikipiki walivamia takriban vijiji vya mbali vinne kwenye eneo la Kanam Jumapili wakipiga risasi watu wakiwemo watoto, na wanaume vijana.

Idadi ya watu waliouwawa katika mfululizo wa mashambulizi ya kutumia silaha kwenye vijiji kadhaa nchini Nigeria katika jimbo la Plateau imeongezeka na kufikia zaidi ya 130.

Watu wenye silaha katika darzeni za pikipiki walivamia takriban vijiji vya mbali vinne kwenye eneo la Kanam Jumapili wakipiga risasi watu wakiwemo watoto, na wanaume vijana.

Maafisa wa polisi na wa ndani wamethibitisha shambulizi hilo lakini hawakutoa idadi ya waliojeruhiwa.

Washambuliaji waliiba mifugo na kuchoma darzeni za nyumba, hali iliyokosesha makazi mamia ya watu na wengine hawajulikani walipo baada ya shambulizi kutokea.

Wakaazi wanalalamika kwamba maafisa wa usalama walichukua karibu saa 24 kufika baada ya shambulizi kutokea.

Wanasema hii ni vurugu mbaya kutokea katika eneo hilo. Nigeria inataabika na wimbi la mashambulizi kutoka kwenye magenge ya watu wenye silaha wanaofanya mauaji mara kwa mara na kuteka watu wakidai malipo ya fidia hasa katika jumuiya ambazo hazina ulinzi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG