Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 21:19

Majaji wa ICC watafakari juu ya kesi ya Ntaganda


Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC Bosco Ntaganda akiwa katika mahakama ya ICC, March 26, 2013.

Mawakili wa Ntanganda wanasema mahakma haina ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi dhidi ya Ntaganda.

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita – ICC, wanatathmini kuona ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kumshitaki Jenerali wa zamani wa Congo Bosco Ntaganda kwa ajili ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Ntaganda alikuwa mahakamani Jumatatu huko The Hague wakati waendesha mashtaka na mawakili wa utetezi walipotoa maelezo yao ya ufunguzi.

Waendesha mashtaka wanamshitaki Ntaganda kwa makosa 18 ikiwemo mauaji, ubakaji na kuwatumia watoto kama wanajeshi katika tuhuma za ghasia zenye ukatili zilizotokea mwaka 2002 na 2003 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mawakili wa utetezi wanadai kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi hiyo.

Ona maoni (2)

mjadala huu umefungwa

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG