Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:18

Maharamia wa Afrika Magharibi wageukia utekaji nyara


Washukiwa maharamia wakiwa kwenye meli ya jeshi la majini la Nigeria baada ya kukamatwa kwa kuliteka jahazi.
Washukiwa maharamia wakiwa kwenye meli ya jeshi la majini la Nigeria baada ya kukamatwa kwa kuliteka jahazi.

Maharamia wa Afrika Magharibi wamegeuka kuwa wateka nyara wakati majeshi ya majini ya kieneo yakiongeza juhudi za kujibu uhalifu wao, ripoti kutoka kundi linalopinga uharamia limesema leo Jumanne.

Ghuba ya Guinea imekuwa eneo hatari sana la maji duniani, huku maharamia wakifanya mashambulizi 54 katika maji yake mwaka jana na kusababisha zaidi ya dola milioni 700 za uharibifu wa uchumi, kwa mujibu wa ripoti kutoka 'Oceans beyond Piracy' yenye makao yake Marekani.

Maharamia hao inaonekana wanabadilisha mbinu wakati majeshi ya majini wamekuwa wazuri katika juhudi za kuwakamata.

XS
SM
MD
LG