Mahakama hiyo imesema kwamba haitasikiliza rufaa iliyowasilishwa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya chini kutoka kwa makundi yanayoshinikiza jina la Trump liondolewe.
Uamuzi huo ni kufuatia ule wa Desemba 19, uliofanywa na mahakama ya Juu ya Colorado iliyogawanyika, ukisema kwamba Trump hafai kuwania urais kutokana na jukumu lake la Jan 6, 2021, kwenye shambulizi dhidi ya jengo la bunge la Marekani.
Uamuzi huo ulikuwa ni mara ya kwanza katika historia ambapo kifungo cha 3 cha marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani kimetumika kumuondoa mgombea urais wa Marekani kwenye uchaguzi.
Kesi za Michigan na Colorado ni miongoni mwa darzeni zinazolenga kuondoa jina la Trump kwenye uchaguzi wa majimbo.
Forum