Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:57

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu yatoa hati ya kumkamata Vladimir Putin


Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) leo Ijumaa imetoa hati ya kumkamata Rais wa Russia Vladimir Putin, ikimshtumu kuwa muhusika mkuu wa uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Moscow ilikanusha mara kadhaa tuhuma kwamba wanajeshi wake walifanya ukatili katika uvamizi wa Russia dhidi ya jirani yake ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

ICC imetoa hati ya kumkamata Putin kwa tuhuma za kuwahamisha kinyume cha sheria watoto na raia wengine wa Ukraine hadi Russia.

Mapema wiki hii, shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba ICC ilikuwa inatarajiwa kutoa hati kadhaa, kwa mara ya kwanza katika uchunguzi wake juu ya mzozo wa Ukraine.

Mahakama hiyo imetoa pia hati ya kumkamata Maria Alekseyevna Lvova-Belova, Kamisheni wa haki za watoto wa Russia, kwa shutma hizo hizo zilizotolewa dhidi ya Putin.

XS
SM
MD
LG