Mahakama ya Katiba ya Thailand imemsimamisha kazi Waziri Mkuu Prayut Chan-O-Cha huku ikiangalia iwapo amefikia mwisho wa muhula wake wa miaka minane.
Uamuzi huo Jumatano ulikuja baada ya vyama vya upinzani kuwasilisha ombi vikipinga Prayut, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya 2014, alikuwa amemaliza muda wake madarakani.
Waziri mkuu wa muda atateuliwa hadi mahakama itakapotoa uamuzi wake katika kesi hiyo.
Miongoni mwa wagombea wakuu wa nafasi hiyo ni Naibu waziri Mkuu Prawit Wongsuwan