Mahakama ya Juu Marekani imemaliza sera ya miongo mingi ya kuruhusu suala la rangi katika elimu ya juu na vyuo vikuu hatua ambayo ilipigiwa kura sita dhidi ya tatu jana Alhamisi, katika kesi iliyowasilishwa na kundi la Students for Fair Admissions, ambao walikishutumu chuo kikuu cha Harvard and Chuo kikuu cha North Carolina Chapel Hill kwa kuwabagua wanafunzi kulinga na rangi zao.
Rais Joe Biden alisema uamuzi huo usibadili lengo la usawa katika elimu ya juu, “wasiachane na nia yao ya dhati kuhakikisha taasisi za wanafunzi zina watu mchanganyiko na ujuzi ambao unaionyesha Marekani kwa ujumla wake.”
Lakini kwa watetezi wengi – baadhi ambao wanasema walihusika moja kwa moja na hatua hii – uamuzi huu ni jambo jema. “Rangi ya ngozi yako isihusike katika lolote hilo. Kwahiyo kama vyyo vitaendelea kuwaangalia wanaotuma mambo kulingana na rangi zao, tutakuwa siyo tu nchi bali tutakuwa nchi yenye kufanya maamuzi kwa upendeleo,” anasema Kenny Xu wa Color us United.
Hatua ya uthibitisho – sera ya kuangalia rangi na asili ya wanafunzi wanaoomba kuingia katika vyuo vya elimu ya juu – imekuwepo tangu miaka ya 1960.
Lengo lilikuwa kuboresha nafasi kwa wanafunzi wanaotuma maombi ambao rangi au asili yao imewaacha na fursa chache za kupata elimu nzuri.
Wachambuzi wameiambia VOA kuwa uamuzi utakuwa na matokeo ya haraka sana. Katherine Meyer wa taasisi ya Brookings anasema, “tunaweza kutarajia kuona kushuka kwa kiasi cha asilimia 10 ya uandikishaji wa watu weusi na wahispania katika taasisi maalum za juu humu nchini aina ya taasisi ambazo huwa zinaangalia rangi kwa sababu kunakuwa na ushindani mkali katika kuomba.”
Katika maoni ya wengi, Jaji Mkuu John Roberts alisema “kuondoa ubaguzi wa rangi kuna maana ya kuondoa yote hayo.”
Mfuasi wa maamuzi ya Mahakama ya Juu Jesse Park anasema,
ni matokeo ya haki kuangalia suala kwa usawa kwa kila mwanafunzi bila ya kujali rangi ya mtu.
Lakini majaji watatu walio wachache alisema maombi kulingana na rangi huenda yataongeza ukosefu wa usawa. Mhitimu mmoja wa chuo kikuu cha Harvard alitoa ushuhuda kwa Mahakama ya Juu kwamba suala la rangi haliwezi kuondolewa kutoka kwa maisha ya mwanafunzi aliyopitia.
Sally Chen, mchina wa Affirmative Action anasema, “nisingekuwa na uwezo wa kueleze hadithi yangu yote kuhusu mimi bila ya kuweka dhana ya rangi na asili. Naweza pia kusema kwamba najivuna kuwa mimi ni Mmarekani mwenye asili ya China, nadhani hilo ni muhimu katika sehemu ya hadithi yangu.”
Juni mwaka 2023 ukusanyaji maoni uliofanywa na Yahoo News/YouGov, ulibaini kuwa kati ya asilia 41 ya wamarekani waliofanyiwa utafiti walisema wanaunga mkono sera isiyoangalia rangi katika kutuma maombi kwenye vyuo vya elimu ya juu.
Forum