Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 12:20

Mahakama ya juu Angola yaamuru kukamatwa kwa mali zenye thamani ya karibu dola bilioni 1 za Isabel dos Santos


Isabela dos Santos mtoto wa rais wa zamani wa Angola na mwanamke tajiri zaidi barani Afrika wakati wa mahojiano yake na Reuters.Januari 9. REUTERS.
Isabela dos Santos mtoto wa rais wa zamani wa Angola na mwanamke tajiri zaidi barani Afrika wakati wa mahojiano yake na Reuters.Januari 9. REUTERS.

Mahakama ya Juu ya Angola imeamuru kukamatwa kwa mali zenye thamani ya karibu dola bilioni 1 za Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, shirika la habari  la Ureno , LUSA lilisema Jumanne.

Hati ya mahakama iliyonukuliwa na Lusa, ya Desemba 19, ilisema mamlaka ilikuwa na ushahidi wa madai ya ubadhirifu na utakatishaji fedha na iliamuru kukamatwa kwa pesa za dos Santos katika "taasisi zote za benki".

Ukamataji huo pia unajumuisha hisa zote za Dos Santos katika kampuni ya Angola ya Embalvidro, pamoja na asilimia 100 ya hisa katika kampuni ya mawasiliano ya simu ya Unitel T+ ya Cape Verde na Unitel STP huko Sao Tome e Principe, kulingana na Lusa.

Jumla ya asilimia 70 ya hisa zake katika kampuni ya mawasiliano ya MStar na Upstar za Msumbiji zinapaswa kukamatwa pia, Lusa ilisema.

Baba yake Dos Santos, Jose Eduardo dos Santos, alifariki mwezi Julai. Alitawala Angola kwa takriban miongo minne hadi mwaka 2017.

Msemaji wa Dos Santos hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Mara kwa mara amekanusha makosa yoyote na aliiambia CNN Ureno mwezi Novemba kwamba mahakama nchini Angola "haziko huru" na kwamba majaji huko "walitumika kutimiza ajenda ya kisiasa".

Amri hyo inakuja baada ya shirika la kimataifa la polisi Interpol kutoa notisi nyekundu kwa Dos Santos mwezi uliopita, ikizitaka mamlaka za kutekeleza sheria duniani kumtafuta na kumkamata kwa muda.

XS
SM
MD
LG