Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 16:41

Mahakama ya Ivory Coast imesitisha mkutano mkuu wa upinzani wa PDCI


Wanachama wa chama cha upinzani nchini Ivory Coast cha Democratic party of the Ivory Coast (PDCI). Ivory Coast, Sept. 24, 2018.
Wanachama wa chama cha upinzani nchini Ivory Coast cha Democratic party of the Ivory Coast (PDCI). Ivory Coast, Sept. 24, 2018.

Amri kutoka kwa jaji katika mahakama ya Abidjan iliyokuwa na tarehe ya Ijumaa na kuonekana na shirika la habari la AFP ilisitisha mkutano ambapo wanachama wa Democratic Party of the Ivory Coast (PDCI) walitarajiwa kuchagua kiongozi mpya wa chama kabla ya uchaguzi wa 2025.

Mkutano mkuu wa upinzani nchini Ivory Coast ulisitishwa dakika za mwisho kwa amri ya mahakama, wakati wajumbe wakijiandaa kumchagua kiongozi mpya leo Jumamosi.

Amri kutoka kwa jaji katika mahakama ya Abidjan, iliyokuwa na tarehe ya Ijumaa na kuonekana na shirika la habari la AFP, ilisitisha mkutano ambapo wanachama wa Democratic Party of the Ivory Coast (PDCI) walitarajiwa kuchagua kiongozi mpya wa chama kabla ya uchaguzi wa 2025.

Wagombea wawili wakuu ni mfanyakazi wa benki, raia wa Ufaransa na Ivory Coast, Tidjane Thiam na Jean-Marc Yace, mwenye miaka 62, meya wa wilaya katika mji mkuu wa kiuchumi Abidjan.

Lakini siku ya Ijumaa jaji aliamuru “kusimamishwa na kuahirishwa kwa mkutano mkuu wa PDCI”, akisema kuwa malalamiko mawili yaliyowasilishwa na wanaharakati yamezingatiwa juu ya shutuma za dosari katika orodha ya washiriki wa mkutano huo.

Forum

XS
SM
MD
LG