Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:04

Mahakama Misri yatoa adhabu ya kifo kwa muuaji wa Kasisi

Maafisa wa Misri walisherehekea kukamilika kwa mradi wa urejeshaji wa miaka 16 wa Kanisa la Coptic la Bikira Maria.Pia linajulikana kama Kanisa linaloning'inia, moja ya makanisa kongwe nchini humo la madhehebu ya Coptic.Ngome ya Kirumi ya karne ya pili.

Mahakama moja ya Misri jana  Jumamosi ilimhukumu mtu mmoja adhabu ya kifo kwa kuuwa kwa  kumchoma  kisu Kasisi wa Kanisa la madhehebu ya  Koptiki  mwezi Aprili katika shambulio lililoshtua taifa hilo lenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.

Nehru Tawfiq, mwenye umri wa miaka 60, alipatikana na hatia katika mahakama ya jinai ya Alexandria kwa mauaji ya Kasisi Arsanious Wadid mwenye umri wa miaka 56 na kupatikana na kisu kinyume cha sheria. Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa mauaji hayo hayakuwa ya makusudi. Tawfiq anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Wadid aliuawa katika eneo maarufu la bahari katika mji wa Alexandria mwezi Aprili.

XS
SM
MD
LG