Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 16:46

Mahakama maalum huko CAR imefanya uamuzi wa kihistoria


Jengo la mahakama maalum katika mji mkuu Bangui huko Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)
Jengo la mahakama maalum katika mji mkuu Bangui huko Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)

Mahakama Maalum ya Jinai, mahakama ya majaji wa ndani na wa kimataifa, ilimhukumu Adoum kifungo cha maisha na wengine miaka 20 baada ya kesi yake ya kwanza kabisa kufanyika

Mahakama moja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) katika uamuzi wa kihistoria siku ya Jumatatu iliwatia hatiani wanamgambo watatu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuwapa vifungo vya jela kuanzia miaka 20 hadi maisha.

Issa Sallet Adoum, Ousman Yaouba na Tahir Mahamat walishtakiwa kwa kushiriki katika shambulizi la kundi lenye silaha la 3R hapo Mei 2019 ambapo wanakijiji 46 kaskazini magharibi mwa CAR waliuawa.

Mahakama Maalum ya Jinai, mahakama ya majaji wa ndani na wa kimataifa, ilimhukumu Adoum kifungo cha maisha na wengine miaka 20 baada ya kesi yake ya kwanza kabisa kufanyika.

Moja ya nchi maskini sana na tete duniani, CAR ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 kwa kiasi kikubwa katika misingi ya kimadhehebu.

Ghasia zilipungua kwa kiwango kikubwa mwaka 2018 lakini mapema mwaka 2021, theluthi mbili ya nchi hiyo iliangukia mikononi mwa makundi yenye silaha yaliyokumbwa na mzozo huo.

XS
SM
MD
LG