Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:18

Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya yatoa  uamuzi wa kihistoria kwa mustakabali wa mashindano ya Super League


Chama cha soka barani Ulaya UEFA
Chama cha soka barani Ulaya UEFA

Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya imetoa  uamuzi wa kihistoria kwa mustakabali wa mashindano ya vilabu vya soka kwamba UEFA na FIFA zilitenda kinyume na sheria ya mashindano ya Umoja wa Ulaya katika kuzuia mipango ya michuano iliyojulikana kama Super League.

Kesi hiyo ilisikilizwa mwaka jana katika mahakama hiyo baada ya Super League kushindwa kuzinduliwa mwezi Aprili 2021. Rais wa UEFA Aleksander Ceferin aliwaita viongozi wa klabu hiyo nyoka na waongo na kutishia kuwapiga marufuku wachezaji kwenye klabu za Super League.

Kundi hilo lililoundwa na vilabu 12 vilivyoasi ambavyo sasa vinaongozwa na Real Madrid na Barcelona pekee baada ya Juventus kujiondoa mwaka huu walichukua hatua za kisheria kulinda nafasi yao na Mahakama ya Haki iliombwa kutoa uamuzi juu ya pointi za kisheria za EU na mahakama ya Madrid.

Vilabu hivyo vilishutumu UEFA kwa kukiuka sheria za Ulaya kwa madai ya kutumia vibaya utawala wake wa soko katika mashindano ya soka.

Forum

XS
SM
MD
LG