Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:24

Magufuli: Vita Vya Dawa za Kulevya ni Jukumu la Serikali


Rais John Magufuli na maafisa watano walioapishwa Ikulu, wakiwemo kamishna wa kupambana na dawa za kulevya na uhamiaji waliosimama nyuma ya rais
Rais John Magufuli na maafisa watano walioapishwa Ikulu, wakiwemo kamishna wa kupambana na dawa za kulevya na uhamiaji waliosimama nyuma ya rais

Rais John Pombe Magufuli, wa Tanzania amesema Jumapili kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya havina budi kuendeshwa na serikali kwa mujibu wa sheria namba tano ya 2015.

Aidha rais amesisitiza kwamba serikali haitahusika katika kuwatetea watanzania 1,007 wanaoshikiliwa kwenye magereza mbali mbali duniani, kwa mashtaka ya dawa za kulevya, pamoja na wafungwa 68 ambao wamehukumiwa kifo Uchina.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:35 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Magufuli alieleza hayo alipokuwa anawaapisha kamishana mpya wa mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Rodgers William Sianga, kamishna mpya wa uhamiaji Anna Peter Makakala na mabalozi watatu Ikulu ya Dar es salaam.

Kiongozi huyo amevitaka vyombo vya usalama na serikali yake kutomwogopa mtu yoyote katika vita hivyo ili kuwaokoa vijana wa Tanzania.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anasema rais ameelezea dhamira yake ya dhati ya kupambana na janga hilo na kwamba serikali yake iko nyuma ya mamlaka husika katika vita hivi, na kwamba hata isiposhinda katika vita hivyo anahakika taifa litafanikiwa kupunguza bishara hiyo haramu kwa kiasi kikubwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemtaka kamishna mpya wa uhamiaji kufanya mabadiliko makubwa ndani ya ofisi hiyo hasa kitengo cha fedha, ili kudhibiti mapato ya serikali pamoja na suala la uhamiaji haramu na utoaji wa hati hewa za kusafiria.

Rais John Magufuli akimapisha kamishna wa Uhamiaji Anna Petre Makakala
Rais John Magufuli akimapisha kamishna wa Uhamiaji Anna Petre Makakala

Kadhalika rais Magufuli pamoja na waziri mkuu Kassim Majaliwa ambaye ndie msimamizi mkuu wa vita hivyo vya kupambana na dawa za kulevya walipongeza juhudi zilizoanzishwa na wakuu wa mikoa katika kupambana na janga hilo kwa lego la kuwaokoa vijana na taifa kwa ujumla.

XS
SM
MD
LG