Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:28

Rais Magufuli ataka kuimarisha ushirikiano na Kenya


Mkutano juu ya biashara kati ya marais wa Kenya na Tanzania mjini Nairobi
Mkutano juu ya biashara kati ya marais wa Kenya na Tanzania mjini Nairobi

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amesema kuwa Kenya ndiyo mshirika wa kibiashara na uwekezaji mkubwa mno wa Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika.

Katika ziara anayoitambua kuwa mkakati wa kuimarisha na kukuza undugu na ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, rais Magufuli, hatimaye aliwasili mjini Nairobi siku ya Jumatatu na kufanya mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Hatimaye wawili hao walihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Nairobi.

Haya yamejiri siku moja tu baada ya ziara ya Rais Kenyatta nchini Sudan.

Katika ziara yake ya kwanza kabisa tangu kuapishwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli na mwenyeji wake wamekubaliana kuharakisha ujenzi wa barabara ya kutoka Bagamoyo nchini Tanzania hadi Malindi, Kenya kuufanya usafiri wa umma kuwa rahisi mno.

Vile vile wawili hao waliwaagiza mawaziri wao wa mambo ya nje kuharakisha juhudi za kubuni tume ya pamoja ya ushirikiano kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kisiasa kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki.

Na Kennedy Wandera

XS
SM
MD
LG