Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 09, 2025 Local time: 11:18

Mradi wa mabasi ya mwendo kasi wazinduliwa rasmi Dar


Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais wa Tanzania, John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli Jumatano ameagiza mamlaka zinazohusika na uendeshaji wa mradi wa mwendo kasi (DART) kuhakikisha unaendeshwa kwa faida.

Rais amesisitiza kuwa ni lazima DART iwe ni chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi mingine ya miundo mbinu wakati akizindua rasmi mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA amesema mradi wa DART jijini Dar es salaam katika awamu yake ya kwanza wenye umbali wa kilometa 20.9 umeigharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 403 ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 317 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Makamu wa rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika, Makhtar Diop yupo mjini Dar es salaam na Jumatano ameshiriki uzinduzi rasmi wa mradi huu ambao ni mkombozi kwa wakazi wanaoishi maeneo yanayopita mabasi haya na yenye msongamano mkubwa wa magari hapo awali.

Rais Magufuli amesema serikali yake inaendelea na jitihada za kutekeleza miradi itakayosaidia kutatua msongamano mkubwa wa magari katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamezungumzia huduma hiyo ya mabasi yaendayo kasi katika jiji la DAR ES SALAAM

Mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka DART, Leonard Lwakatare amesema wakati wa uzinduzi wa mradi wa mabasi hayo tayari walikuwa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 800.2 na kiasi hicho kilipanda mwezi Disemba mwaka jana kufikia shilingi bilioni 3.39.

XS
SM
MD
LG