Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 09:24

Mageuzi yahitajika katika bandari ya Dar es Salaam


Makontaina kwenye bandari ya Dar es Salaam, Tanzania
Makontaina kwenye bandari ya Dar es Salaam, Tanzania
Benki Kuu ya Dunia imetoa ripoti ya kwanza ya mwakqa huu juu ya hali ya uchumi wa Tanzania kwa kuzingatia umuhimu wa bandari ya Dar es Salaam katika mendeleo ya uchumi wan chi hiyo na mataifa jirani.

Ripoti hiyo inapendekeza mageuzi muhimu katika bandari hiyo ili kuweza kuimarisha uchumi na kuongeza mapato ya wastani ya uzalishaji - GDP ya Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki.

Waatalamu wa Benki Kuu ya Dunia kwa kushirikiana na maafisa wa serikali na wadau wa masuala ya kiuchumi hutoa ripoti hiyo kila baada ya miezi sita baada ya kutathmini na kuchunguza hali ya uchumi wa Tanzania kwa kuzingatia maada maalum kila kipindi.
Kuimarishwa bandari ya Dar es Salaam - 7:15
please wait

No media source currently available

0:00 0:07:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mchumi mwandamizi wa Benki Kuu ya Dunia mjini Dar es Salaam, Josphate Kweka anasema, kuna masuala matatu walozingatia kujua umuhimu wa bandari hiyo katika uchumi jumla wa Tanzania na mataifa jirani yanayo tumia bandari hiyo.

“La kwanza ni kwamba unaweza kuangalia umuhimu huo kwa kuangalia hasara ambayo nchi inapata licha ya kwamba kuna nchi za jirani ambazo zinategemea hii bandari na zinaathirika kutokana na ufanisi mdogo katika hii bandari.”

Utaratibu huu unawasaidia maafisa wa serikali na wadau husika kuchukua hatua kutokana na mapendekezo ya ripoti hiyo. Jaffer Machano mjumbe katika bodi ya mamlaka ya bandari Tanzania anasema mageuzi muhimu yameanza kutekelezwa ili kuweza kuimarisha huduma za bandari hiyo.

“Mageuzi yanayotokea sasa hivi ni mambo mawili mpaka matatu, la kwanza ni kuongeza ufanisi kwa kujaribu kuongeza miundo mbinu ya bandari ya Dar es Salaam. Kwa kuweka bandari kavu kisarawe, kuweka reli ya kuchukua mizigo moja kwa moja kufikia Kisarawe.”

Hii anasema itapunguzamsongamano wa meli kukaa nje ya bandari kwa siku 10 kama ilivyoelezwa kwenye ripoti. Pili Machano anasema ni kuongeza miundo mbinu ya teknohama ili sweta zote za serikali zinazohusiana na kazi za bandari ziweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mbali na mageuzi hayo muhimu ya miundombinu ripoti inazungumzia matatizo ya uzembe, kupotea mali na ulaji rushwa mambo yanayiorudisha nyuma maendeleo ya uchumi.

Kwa ujumla hata hivyo, ripoti na maafisa wanaeleza matumaini mazuri ya kufanyika mageuzi kutokana na kuwepo na utashi wa kisiasa wa kuleta mabadiliko na mageuzi yanyofanyika hivi sasa ni ya kutia moyo wanasema.
XS
SM
MD
LG