Wawili kati ya wapiganaji waliouwa walikuwa maafisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo la wapiganaji.
Jeshi la Marekani limesema kwamba lilitekeleza mashambulizi hayo kaskazini mwa Syria jumanne, yaliyolenga maafisa wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Hurras al-Deen, lenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, na makundi mengine nane.
Wametangaza pia shambulizi jingine la Septemba 16, la kiwangi kikubwa, dhidi ya kambi za kundi la kigaidi la IS katika sehemu ya kijijini katikati mwa Syria, na ambalo liliua wapiganaji 28 wakiwemo viongozi wao wanne wa Syria.
Kuna karibu wanajeshi 900 wa Marekani nchini Syria wanaojaribu kuzuia kundi la kigaidi la Islami state kujiimarisha. Kundi hilo lilikuwa limedhibithi sehemu kubwa ya Iraq na Syria mwaka 2014.
Forum