Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 18:26

Mafuriko yaua watu 30 nchini Nigeria


Shamba la mpunga lililokumbwa na mafuriko huko Makurdi, nchini Nigeria, Oktoba 1, 2022. Picha ya Reuters
Shamba la mpunga lililokumbwa na mafuriko huko Makurdi, nchini Nigeria, Oktoba 1, 2022. Picha ya Reuters

Mafuriko makubwa katika mji wa kaskazini mashariki mwa Nigeria yameua watu 30 na kulazimisha wengine 400,000 kuhama makazi yao, maafisa walisema Jumatano.

“Idadi ya vifo ni 30, msemaji wa idara ya kitaifa ya kusimamia majanga (NEMA) Ezekiel Manzo aliiambia AFP, siku moja baada ya maji kutoka kwenye bwawa lililojaa kusomba maelfu ya nyumba katika mji mkuu wa jimbo la Borno.

Mfanyakazi mwingine wa idara hiyo, Zubaida Umar alisema “Hali huko Maiduguri inatisha sana.”

Alisema mafuriko yaliteketeza asilimia 40 ya mji wote, na watu walilazimika kuondoka kwenye nyumba zao na wametawanyika kila mahali.

Umar alisema takwim walizonazo ni kwamba kuna watu 414,000 waliohama makazi yao.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi nchini Nigeria lilisema Jumanne kwenye mtandao wa X kwamba mafuriko hayo yalikuwa moja ya mafuriko mabaya kuukumba mji huo katika kipindi cha miaka 30.

Forum

XS
SM
MD
LG