Karibu watu nusu milioni wamelazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko nchini humo, huku maisha ya wengine milioni 1.2 yakiathiriwa, waziri wa Habari Daud Aweis amesema wakati akizungumza na wanahabari mjini Mogadishu.
Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, na ambayo tayari imetoa dola milioni 25 za kusaidia kutokana na athari za mafuriko hayo, wiki iliyopita ilieleza mafuriko yanayoendelea Somalia kama tukio la karne, litakalokuwa na athari kubwa za kibinadamu.
OCHA ilisema kwamba ingawa hatua zote zinachukuliwa, mafuriko ya kiwango hicho hayawezi kuzuilika, na kwa hivyo kupendekeza onyo la mapema pamoja na kuchukuliwa kwa tahadhari, ili kuokoa maisha.
Forum