Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:48

Mafuriko yaua na kuwafurusha wengi nchini Sri Lanka


People play on a flooded road after they moved out from their houses in Biyagama, Sri Lanka.
People play on a flooded road after they moved out from their houses in Biyagama, Sri Lanka.

Chama cha msalaba mwekundu nchini Sri Lanka kinasema karibu familia mia mbili nchini humo zinaripotiwa kupotea na hofu kubwa ni huenda wamezikwa kwenye tope kufuatia mvua kali zilizosababisha mafuriko.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa mtandao, chama cha msalaba mwekundu nchini humo kimeeleza kwamba timu za uokozi zilielekea eneo la tukio mapema leo pamoja na maafisa wengine wa serikali na walifanikiwa kuokoa watu 180, licha ya kukatika kwa umeme katika vijiji vya Siripura, Pallebage, na Elagipitya mjini Aranayake katika wilaya ya Kagalle.

Chama hicho cha msalaba mwekundu kinasema kiliokoa maiti 13. Mvua imesababisha mafuriko katika miji kadhaa ikijumuisha Colombo. Shule nchini kote zimefungwa leo hii kwa sababu ya mvua.

Kituo cha maafa cha Sri Lanka kimeripoti watu 11 kufariki dunia kwa umeme na mmomonyoko mdogo wa udongo katika siku za hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG